<p style='right: 0px; position: fixed; text-align: right; bottom: 0px;'>
Loading...
YANGA YAZIDI KUMEGWA, MCHEZAJI MWINGINE KUTAMBULISHWA AZAM LEO - TEAMTZ- Everything Eclusive

Breaking News

YANGA YAZIDI KUMEGWA, MCHEZAJI MWINGINE KUTAMBULISHWA AZAM LEO


Vuguvugu la usajili kwa wachezaji wa soka nchini Tanzania linaendelea kama kawaida ambapo klabu ya Azam FC inatarajiwa kumtambulisha beki namba mbili wa Yanga, Juma Abdul.

Mchezaji awali alitakiwa kutambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari wiki iliyopita lakini badala yake akatambulishwa kocha Hans van der Pluijm pekee.

Ofisa wa Habari wa Azam, Jaffar Maganga, mapema baada ya kumtangaza Plujim kuwa kocha wao mpya, alifunguka na kueleza Jumatatu itakuwa siku rasmi ya kulipua bomu jingine.

Endapo Abdul atatangazwa leo na Azam FC, atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam ndani ya mwaka huu baada ya Mzimambwe, Donald Ngoma.


Taarifa za chini zinaeleza tayari Azam wamemalizana na Ngoma na inaelezwa ameshaini mkataba wa miaka miwili.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();