<p style='right: 0px; position: fixed; text-align: right; bottom: 0px;'>
Loading...
YANGA YAAMBULIA M6 ZA SPORTPESA SUPER CUP - TEAMTZ- Everything Eclusive

Breaking News

YANGA YAAMBULIA M6 ZA SPORTPESA SUPER CUP

Timu ya soka ya Yanga imeondoshwa rasmi kwenye mashindano ya SportPesa Super Cup 2018 baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Kakamega HomeBoys ya Kenya.
Mashindano hayo yalifunguliwa leo yatafikia kikomo June 10 mwaka huu na bingwa atapata nafasi ya kwenda kwenye Jiji la Liverpool kucheza na klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza maarufu kamaEPL.
Mabao ya Kakamega yamefungwa na mshambuliaji wao Allan Wanga katika dakika 25, na 30 huku bao la 3 likiwekwa kimiani na Wycliffe Opondo katika dakika ya 85.
Bao pekee la Yanga limefungwa na Matheo Anthony katika dakika 33 kwa mpira wa faulo, baada ya ushindi huo Kakamega wanasonga mbele katika hatua ya Nusu Fainali huku Yanga ikiyaaga rasmi mashindano hayo.
Pamoja na kundoshwa kwenye mashindano hayo klabu ya Yanga imeambulia dola 2500 sawa 6M kama mshikiri wa mashindanl hayo kwa mjibu wa waandaa mashindano Sportpesa.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();