<p style='right: 0px; position: fixed; text-align: right; bottom: 0px;'>
Loading...
Azam yaifirisi tena Yanga, yataraji kufanya usajili huu - MICHEZO NA BURUDANI BLOG

Breaking News

Azam yaifirisi tena Yanga, yataraji kufanya usajili huuLeo Jumatatu Juni 4 2018, klabu ya Azam inatarajia kumtangaza mchezaji mpya atakayesaini mktaba na klabu hiyo.

Mchezaji huyo anatajwa kuwa ni kitasa cha kulia cha klabu ya Yanga Juma Abdul ambapo utakuwa ni mwendelezo wa kusajili wachezaji kutoka kwenye klabu hiyo ambayo imekaa kimya kuhusu suala la usajili.

Jaffar Maganga , Ofisa wa Habari wa Azam amueleza mwandishi habari hizi kuwa  Jumatatu itakuwa siku maalumu ya kulipua bomu jingine.

Endapo Abdul atatangazwa leo na Azam FC, atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam ndani ya mwaka huu baada ya Mzimambwe, Donald Ngoma.