<p style='right: 0px; position: fixed; text-align: right; bottom: 0px;'>
Loading...
MSHAHARA WA SALAMBA SIMBA USIPIME, Cheki Hapa.... - MICHEZO NA BURUDANI BLOG

Breaking News

MSHAHARA WA SALAMBA SIMBA USIPIME, Cheki Hapa....

Imefahamika kuwa mshambuliaji tegemeo wa Lipuli FC, Adam Salamba, atapokea mshahara wa shilin­gi milioni mbili kwa kipindi cha miaka miwili ambacho ataichezea Simba, ambao ni sawa na shilingi milioni 48 kwa mkataba wake wote.
Mshambuliaji huyo alisaini mkataba huo wa miaka miwili juzi akitokea Lipuli ambayo ilimu­uza baada ya Yanga na Azam FC kushindwa kuinasa saini ya nyota huyo wa kupachika mabao.

Salamba aliyemaliza msimu na mabao sita, anatarajia kuungana na mshambuliaji wa Majimaji FC ya Ruvuma, Marcel Boniventure aliyefunga mabao 14 kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata gazeti la Championi, Salamba alisaini mkataba huo wa miaka miwili kwa dau la shilingi milioni 40.
Mtoa taarifa huyo alisema, katika dau hilo la usajili lililotolewa na Simba, shilingi milioni 25 zilik­wenda kwa timu yake ya zamani ya Lipuli, iliyommiliki kwa ajili ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea timu hiyo.
“Uongozi wa Lipuli ni lazima unu­faike na mauzo ya Salamba, kama unavyofahamu mchezaji alikuwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea Lipuli.
“Hivyo, kabla ya mchezaji huyo kusaini mkataba, yalifanyika mazungumzo kati ya sisi timu tunaommiliki mchezaji, mchezaji mwenyewe na uongozi wa Lipuli kwa ajili ya kukubaliana baadhi ya vitu ikiwemo kupata sehemu ya fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja katika dau hilo la usajili.
“Uzuri ni kwamba hayo yote yalifanyika na kufikia muafa­ka kuwa sisi Lipuli tupatiwe shilingi milioni 25 za kusi­tisha mkataba wa Salamba pamoja na makubaliano mengine ya bin­afsi kati ya mche­zaji na uongozi wa Simba.