<p style='right: 0px; position: fixed; text-align: right; bottom: 0px;'>
Loading...
JEURI YA PESA YAZIDI KUWATESA YANGA SASA DANTE ATIMKIA SIMBA KWA KWANJA MREFU - TEAMTZ- Everything Eclusive

Breaking News

JEURI YA PESA YAZIDI KUWATESA YANGA SASA DANTE ATIMKIA SIMBA KWA KWANJA MREFU
Taarifa za uhakika za wazi kabisa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinadai kuwa beki wao kisiki Andrew Vicent ‘Dante’, mkataba wake umemalizika rasmi juzi Jumatatu baada ya mchezo wao na Azam FC, hivyo yuko huru kucheza timu yoyote itakayoweza kummwagia fedha.

Msimu huu uliofikia tamati juzi Jumatatu Dante alionekana kuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga tofauti na msimu wa kwanza alipojiunga na timu hiyo pamoja na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Dante amesema, kwa sasa yuko huru kufuatia mkataba wake huo kumalizika na kwamba, hadi sasa hajazungumzia suala lolote la kuongeza mkataba na Yanga.

“Nipo huru tangu Jumatatu ligi ilipofikia mwisho na mkataba wangu nao ulifikia mwisho, hivyo hadi sasa sijaongea na yeyote kuhusu kuongeza mkataba mpya zaidi nangojea kama uongozi utasema lolote ili niweze kumalizana nao japo kuna dili zangu nyingine ambazo nazisikilizia,” alisema Dante.
'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();