<p style='right: 0px; position: fixed; text-align: right; bottom: 0px;'>
Loading...
AZAM FC YAANZA MAZUNGUMZO NA BEKI WA YANGA ALIYEMALIZA MKATABA - MICHEZO NA BURUDANI BLOG

Breaking News

AZAM FC YAANZA MAZUNGUMZO NA BEKI WA YANGA ALIYEMALIZA MKATABA


KIKOSI CHA AZAM FC HADI MSIMU WA 2015-16, KILIVURUGIKA KWA WAKONGWE KADHAA KUONDOKA AKIWEMO JOHN BOCCO.

Azam FC inaonekana kuendelea kujiimarisha zaidi katika usajili kwa ajili ya msimu mpya wa 2018-19 kwa kuwa tayari imejipanga kuimarisha safu yake ua ulinzi.

Taarifa zinaeleza, Azam FC imeanza mazungumzo na beki mmoja wa pembeni wa Yanga ikitaka atue Chamazi.

Taarifa zinaeleza, beki huyo anaweza kumwaga wino usiku wa leo au kesho kwa kuwa anaonekana amekubaliana na Azam FC.

"Kweli kuna mazungumzo lakini si suala la kulizungumzia kwa kuwa halijakamilika," kilieleza chanzo kutoka Azam FC.

Lakini kutoka ndani ya Yanga, taarifa zilieleza kwamba wanajua kuwa beki huyo ana mazungumzo na Azam FC.

"Tunalijua hilo, lakini sasa hatuna ujanja. Acha tusubiri kwanza kwa kuwa tunajaribu kuwasiliana naye na kujua cha kufanya.

"Kweli tunajaribu kufanya kila kinachowezekana kadiri ya uwezo wetu lakini mambo hayajawa mazuri."

Mambo yameshindwa kuwa wazi kwa kuwa kila klabu imekuwa ikifanya siri suala la usajili kuhofia kupokwa wachezaji na hasa Simba na Azam FC wamekuwa wakichuana sehemu kadhaa katika suala hilo la usajili.