Breaking News

Msanii Mh TEMBA amefutiwa kesi yake ya kutishia kuua, soma zaidi hapa

MAHAKAMA ya Mwanzo Temeke, jijini Dar es Salaam, imemuachia huru msanii wa muziki wa kizazi kipya, Amani James (33), maarufu kama Mheshimiwa Temba, aliyekuwa anakabiliwa na mashitaki ya kutishia kuua kwa kutumia kisu kutokana na wivu wa kimapenzi baada ya mlalamikaji kuona hana haja ya kuendelea na kesi.  Kesi hiyo namba 371 ya mwaka huu ilisomwa kwa mara ya kwanza febuari 25, mwaka huu mbele ya Hakimu Cloudia Frank wa mahakama hiyo.  Hata hivyo, mshitakiwa huyo baada ya kusomewa mashitaka yake aliachiwa kwa dhamana hadi machi 11, mwaka huu.  Kwa mujibu wa chanzo chetu machi 9, mwaka huu siku mbili kabla ya kutajwa kwa kesi hiyo, mlalamikaji Godfrey Deogratius maarufu kama Sulla aliomba mahakama ifute kesi hiyo kwa vile hana nia ya kuendelea nayo  SOURCE: https://www.facebook.com/photo.php?fbid=877907758919310