Breaking News

Kutana na Kala Jeremiah akizungumzia ngoma yake mpya"Nchi Ya Ahadi"

Star wa Hip Hop Kala Jeremiah amezungumzia track ya ‘Nchi ya Ahadi’ aliyomshirikisha ROMA, amesema idea ya wimbo ni wazo la siku nyingi haihusiani na uchaguzi wa mwaka huu ila amejaribu kuwakumbusha watu kujitokeza kujiandikisha kupiga kura ili waweze kujipatia kiongozi sahihi.

Kwa upande wake ROMA ambae ameshirikishwa amesema wimbo huo aliandikiwa na Kala na hakukuwa na ugumu wowote kwa sababu haikuwa mara yake ya kwanza kufanya nae kazi.