Breaking News

Jux, Nahreel na Iyanya waingia gym kupasha, ni collabo mpya?

Mwaka huu Jux ana spidi kali. Baada ya kutoka kushoot video ya wimbo aliomshirikisha Joh Makini (haujatoka) nchini Afrika Kusini, muimbaji huyo huenda akawa anatengeneza collabo na msanii wa Nigeria, Iyanya. Muimbaji huyo ambaye wiki iliyopita aliachia video ya wimbo wake mpya ‘Nikuite Nani’ amepost picha akiwa na Iyanya na producer Nahreel.