Breaking News

Haya ni maneno ya Ney Wa Mitego kuhusiana na collabo yake na Diamond Platinumz inayokujia hivi karibuni...

Msaniii Nay wa Mitego ambae kwa sasa bado anahit na ngoma yake ya Akadumba amefunguka na kusema kuwa mashabiki wa Ney na Diamond Platnumz wakae mkao wa kula kwani mzigo wao mpya muda wowote ndani ya wiki hizi mbili unashuka,


Nay wa Mitego amesema hayo na kusisitiza kuwa anadhani wimbo huo wa sasa huenda ukawa ni wimbo mkubwa kuliko wimbo wa awali waliotoa wakali hao unaofahamika kama Muziki gani.


Nay wa Mitego amesema kuwa kutokana na matatizo yake ya kifamilia ndiyo yamechelewesha kukamilishwa kwa wimbo huo lakini kwa kuwa amesharudi na kutatua hayo matatizo hivyo ngoma inamaliziwa siku mbili hizi na kisha baada ya hapo mipango ikaa sawa siku yoyote ngoma hiyo itatoka ili kuwapa raha mashabiki zao.


"Yeah kuhusu ngoma hiyo naweza kusema ipo tayari ingawa mimi kuna vitu kidogo bado sijavimalizia kutokana na ukweli kwamba siku mbili tatu zilizopita nilikuwa na matatizo ya kifamilia hivyo nilipata dharula nikasafiri na sasa nimerudi hivyo nitamalizia na kila kitu kikienda sawa hiyo ngoma itawafikia mashabiki zetu,Nadhani ngoma hiii inaweza kuwa kubwa zaidi ya ngoma yetu ya awali ya Muziki gani hivyo wategemee kitu kizuri kutoka kwa Nay na Diamond Platnums"


Mkali huyo wa michano ambae mpaka sasa anawatoto watatu amefunguka na kuweka wazi kuwa ni kweli hana mahusiano ya kimapenzi tena na aliyekuwa mchumba wake Siwema pia hana mpango wa kuwa katika mahausiano ya kimapenzi bali mapenzi yake amehamishia kwa watoto wake watatu ambao hao ndio wanampa nguvu zaidi ya kuzidi kutafuta pesa na kuwajengea maisha ya baadae.