Breaking News

Haya ni maneno ya Ben Pol kwa kuichelewesha video ya ‘Sophia’?

Ben Pol weekend hii anatarajia kufanya show ya usiku wa ‘Sophia’ ndani ya Dodoma, safari yake Dom itaunganisha pia zoezi la kushoot video ya wimbo wa mkali huyo ambao anasema mipango ilikuwa video ifanywe siku nyingi zilizopita lakini baada ya fans kuipokea vizuri audio aliona aongezee fungu la bajeti ya video hiyo.

Show yake hiyo atasindikizwa na kundi la Weusi pamoja na mwanamama Khadija Kopa.

Ben amesema kwenye event hiyo fans watashuhudia Sophia akivishwa pete ya uchumba na show hii ni shukrani yake kwa fans wa Dom kuipokea vizuri track yake ya ‘Sophia’.