Breaking News

Soma hapa kupata taarifa zaidi kuhusiana na kifo cha Mbunge wa Mbinga KAPTENI JOHN KOMBA

Mbunge wa Mbinga Mh. Kapten John Komba amefariki dunia leo saa kumi jioni katika hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa mtoto wa marehem Jerry Komba,amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach.

Miaka mitatu iliyopita, Komba alipelekwa nchini India alikokwenda kufanyiwa upasuaji kwenye nyonga, tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu likichagizwa na ule unene aliokuwa nao.
Katibu wa mbunge Gasper Tumaini alisema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ na ndipo mauti yalipomkuta.


Katibu huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hosp ya Lugalo jijini Dar Es salaam ambapo ratiba ya maziko bado haijafahamika.